Kwa mujibu wa Sheria, mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 haruhusiwi kusimamia au kutoa burudani katika harusi kuanzia saa moja usiku.
Ni muhimu maharusi na waendesha sherehe kujiridhisha umri wa wadada na wakaka wanaowasindikiza maharusi au kutoa burudani wakati wa usiku ili kuona kama wamekidhi umri wa kushiriki sherehe wakati wa usiku. Maana kutokujua sheria sio sababu ya kukufanya usitiwe hatiani. Hakikisha umri wao ume miaka 18 au zaidi.