Sheria ya Ndoa, kifungu cha 63(1) kimeweka jukumu kwa mume kumpatia mke wake sehemu nzuri ya kuishi. Sasa kama nyumba ambayo mke anaishi ni ya kupanga, basi jukumu la kulipa kodi ya nyumba hiyo ni la mume peke yake. Sheria haimlazimishi wala haijampatia mke jukumu la kuchangia au kumsaidia mume wake katika hilo.

Jukumu la mume kulipa kodi ni kwenye nyumba ambayo mke wake anaishi bila kujali kama na yeye mume anaishi hapo au anaishi sehemu nyingine.